THE MOST FROM THE COAST !

..


 Coastweek website


XINHUA NEWS SERVICE REPORTS FROM THE AFRICAN CONTINENT

 

Kiswahili watambaa kama kobe makini

(Miaka 50 ya kushrehekea Kiswahili)

.
 I am submitting a poem called: Kiswahili watambaa kama kobe makini. The poem was presented during the
50 years celebrations of Kiswahili as a national and official language of Kenya and Tanzania. The celebrations
were organised by the embassies of Kenya, Tanzania, Burundi and Democratic Republic of Congo (DRC) in
Stockholm, Sweden. - Dr. Ahmed Faris, Associate professor (Bacteriology, Microbiology), Stockholm.

.

Kiswahili watambaa kama kobe makini | Coastweek

Shairi lilitolewa Stockholm (Sweden) katika sherehe iliyoandaliwa
na mabalozi wa Kenya, Tanzania, DRC na Burundi - Ahmed Faris

 

1. Kiswahili ulizaliwa Shungwaya pwani

ukatambaa toka mwambao Somalini

na kuwapa wengi wa pwani na visiwani

hongera! watambaa kama kobe makini

 

2. Wamvita, -Ngazidja, -Lamu na -Tangani

Wameweza, wakikutana mabarazani

lahaja hizo si vizuizi safarini

hongera! watambaa kama kobe makini

 

3. Kutoka mwambaoni huko mizizini

nako Uganda na Burundi ukaingia ndani

na ulipowasili mipaka ya Kongoni

hongera! watambaa kama kobe makini

 

4. Na Waruwanda kukutumia kaulini

khususan wanapokukutumia nyimboni

kunapotolewa mawaidha ya kidini

hongera! watambaa kama kobe makini

 

5. Umekataa kujitenga mwambaoni

na Wamalawi walikutoa ugenini

jumla wanaokutumia kaulini

hongera! watambaa kama kobe makini

 

6. Kenyatta ´litumia Kikikuyu nyumbani

lakini alipofungwa huko gerezani

Kiswahili alikutumia kifungoni

hongera! watambaa kama kobe makini

 

7. Pindi tu Kenyatta kutolewa pinguni

naye hakusita kukutumia hadharani

hotuba alizitoa kivyako nchini

hongera! watambaa kama kobe makini

 

8. Na katika baraza la taifa nchini

ili upewe taji la kudumu mikowani

na utumiwe na watu wote taifani

hongera! watambaa kama kobe makini

 

9. Leo watumiwa ofisini na shuleni

Hamisi, Toni na Pateli huko sokoni

naye mzungu Joni wa kutoka Englani

hongera! watambaa kama kobe makini

 

10. Changanyiko lako na Kingereza msemoni

na uingiliaji wa lugha nyingine Shengeni

huko vijana huitumia kiurafikini

hongera! watambaa kama kobe makini

 

11. Vijana wa Tanzania barabarani

huu upya wa usemaji masikanini

he wee! antena na bukani kimtaani

hongera! watambaa kama kobe makini

 

12. Serikali ya Moi nisikie mwandani

maziwa yalotolewa bure mashuleni

nyayo hichi na nyayo kile serikalini

hongera! watambaa kama kobe makini

 

13. Na Nyerere, taji lako Tanzaniani

nayo filosofia ujamaa siyasani

maelezo baada habari redioni

hongera! watambaa kama kobe makini

 

14. Zaidi yalotajwa hapo mwanzoni

inayotokea kiwaziwazi nyimboni

kama Wainaina “Twende Twende” nyimboni

hongera! watambaa kama kobe makini

 

15. Tarabu za Kimvita na -tanzaniani

na nyimbo za Kikongo Kiswahilini

Lolilo naye huko Burundi densini

hongera! watambaa kama kobe makini

 

16. Naye Khadja Nin kutoka Burundi amini

kwa hiyo sauti yake ya furaha nyimboni

hata humpa mtu mawazo fikirani

watambaa kama kobe makini

 

17. Utumiaji wa Kiswahili nyimboni

nyimbo tunazosikia barabarani

zimekuwa shule kotekote hadharani

hongera! watambaa kama kobe makini

 

18. Kuhifadhi nyimbo kimoyoni

nazo hututambaa mwetu bongoni

punde si punde hutoka midomoni

hongera! watambaa kama kobe makini

 

19. Mhamihaji naye alipo masikani

hulazimika kukutumia ugenini

pindi kurudi nyumbani mizizini

hongera! watambaa kama kobe makini

 

20. Wakati wa vita vikuu ulimwenguni

yaliyotaka lugha moja ulinzini

kwa wote kutumia lugha moja kazini

hongera! watambaa kama kobe makini

 

21. Wetu walo Ulaya na Uamerikani

wamefatwa na wengine ulimwenguni

wakikutana huko walipo ugenini

hongera! watambaa kama kobe makini

 

22. Ufundishaji Kiswahili Ujerumani

kashika Sleman Saidi huko Berlini

wao walikuangaza kwa Mjarumani

hongera! watambaa kama kobe makini

 

23. Nayo masomo ya Kiswahili Marekani

 na vyuo vikuu vingi ulimwenguni

vimetupa profesa kadha Kiswahilini

hongera! watambaa kama kobe makini

 

24. Na Said Ahmed Mzanzibari ugenini

kafatwa na Profesa Lioba (Moshi) Amerikani

lugha inayosongea mbele duniani

hongera! watambaa kama kobe makini

 

25. Kiswahili, lugha njema yami utotoni

nikutumiacho na wenzangu Uswidini

si mbali sana na kwako mizizini

kunako wengi wa watu kwa milioni

 

Harambee! tia kasi sana mwendoni

 

kati ya watu wachache humo vijijini

kulekea Msumbiji kiamani

utamaduni rasmi wa uswahilini

la, huna dhamiri ya kurudi nyumbani

 

kutumia lahaja mbalimbalini

kufahamiana kimazungumzoni

waliko- na wanakokwenda mbeleni

la, huna dhamiri ya kurudi nyumbani

 

ukapelekwa bara na walio biasharani

kama chombo thabiti cha mazungumzoni

ukapokelewa vivyo hivyo manenoni

la, huna dhamiri ya kurudi nyumban

 

ni dalili ya urahisi wako lughani

na humo misikitini na makanisani

baina ya wafuasi wanaoamini

la, huna dhamiri ya kurudi nyumbani

 

bali ulijitambaza bara Zambiani

na kukukaribisha kwingi majumbani

ni milioni mia moja na hamsini5

la, huna dhamiri ya kurudi nyumbani

 

kuwa lugha ya wazazi wake Kikuyuni

kwa kuutaka uhuru wa Kenya nchini

kwa miaka tisa na wenziwe jelani

la, huna dhamiri ya kurudi nyumbani

 

uraisi wa Kenya alipewa shereheni

huko Kenya ya makabila karibu hamsini

baada chanzo chake Harambee jamani

la, huna dhamiri ya kurudi nyumbani

 

Kenyatta kakupigania kibavuni

kwa kufanywa lugha ya kitaifa nchini

iliyo na lugha zizidizo sitini

la, huna dhamiri ya kurudi nyumbani

 

na huko misikitini na makanisani

wakutumia wakiwa shughulini

amejifunza sababuye akutumie kazini

la, huna dhamiri ya kurudi nyumbani

 

limekupa umbo la Shengi vichochoroni

umeongeza lahaja mpya mitaani

pasi wazazi kujua wanasema nini

la, huna dhamiri ya kurudi nyuma

 

wamekubuni kivyao kama wa Kenyani

waitwa kirasmi lugha ya mitaani

ni sikio na soma sana tukibaini

la, huna dhamiri ya kurudi nyumbani

 

iliitwa Serikali ya Nyayo nchini

´lijulikana Maziwa ya Nyayo jamhurini

dalili ya muhimu wako mwongozoni

la, huna dhamiri ya kurudi nyumbani

 

alikuvisha mapema huko bungeni

ilikueneza kotekote vijinini

yalikupambisha kwa vicheko mikahawani

la, huna dhamiri ya kurudi nyumbani

 

nakuongezea uijuwe yako thamani

tukisikia waimbaji mijijini

katumia Shengi kwa fahari na nishani

la, huna dhamiri ya kurudi nyumbani

 

zatia raha na tabasamu miyooni

zina midundo ya kuvutia gitarini

astarehesha na wimbo hitaji CD-ini

la, huna dhamiri ya kurudi nyumbani

 

Lo! atuimbia sina mali sina deni

huifanyisha damu moto moto mwilini

imbapo mimi “I'm free, kama maji[ni] “hongera!

la, huna dhamiri ya kurudi nyumbani

 

umekupeleka mbali ya mipakani

kama Bongo Flava humo daladalani

hufunza lugha mchana na usikuni

la, huna dhamiri ya kurudi nyumbani

 

ni johari tunayochukua njiani

naposikilizwa mara kwa mara makini

tunapojiona peke yetu faraghani

la, huna dhamiri ya kurudi nyumbani

 

unakokutawala kilugha mijinini

apate ishi na wenyeji ukarimuni

huwa paka `hamisha kipaka mdomoni

la, huna dhamiri ya kurudi nyumban

 

ukatumiwa kusaidiya majeshini

sababu ya makabila mengi vikosini

ulinzi ulirahisishwa vitani

la, huna dhamiri ya kurudi nyu

 

kuyatafuta maisha bora ugenini

kutimiliza matakwa yao duniyani

Kiswahili huwagandisha ujamaani

la, huna dhamiri ya kurudi nyumbani

 

kabla vita vya kwanza ulimwenguni

kabla ya Mtoro Bakari hapo mjini

aliyetaka jifunza kwake mkoloni

la, huna dhamiri ya kurudi nyumbani

 

pamoja na Uingereza na Ujerumani,

vinavyosomesha Kiswahili ng´amboni

kama ustadh Azizi Lodhi Uswidini

la, huna dhamiri ya kurudi nyumbani

 

bingwa wa Kiswahili Ujerumani

kunakofunzwa Kiswahili kimoyoni

baada ya kupewa rutuba mwanzoni

la, huna dhamiri ya kurudi nyumbani

 

umenilea Ahmedi Farisi chomboni

na napokwenda Mombasa mitaani

ulikotoka kuingia ulimwenguni

zaidi ya wale wachache Shungwayani

 

yako safari haijafika kikomoni


CLICK HERE:

DOWNLOAD WORD DOCUMENT OF THIS POEM TOGETHER WITH ANNOTATIONS AND FULL REFERENCES

Remember: you read it first at coastweek.com !


http://micekenya.co.ke

 

TO ADVERTISE ON THIS WEB SITE:  www.coastweek.com
Please contact

MOMBASA - GULSHAN JIVRAJ, Mobile: 0722 775164 Tel: (+254) (41) 2230130 /
Wireless: 020 3549187 e-mail: info@coastweek.com

NAIROBI - ANJUM H. ASODIA, Mobile: 0733 775446 Tel: (+254) (020) 3744459
e-mail: anjum@asodia.co.ke

 
    © Coastweek Newspapers Limited               Tel: (+254) (41) 2230130  |  Wireless: 020 3549187  |  E-mail: info@coastweek.com